Siasa na Uchumi

SERIKALI YAAJIRI WATUMISHI WA KADA YA AFYA.

Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetoa nafasi za ajira kwa wananchi wote waliosomea taaluma hiyo. Kwa maelezo zaidi bofya link hizi hapa chini

LINK 1. (http://www.moh.go.tz/index.php/newsroom/195-tangazo-la-ajira-kada-ya-afya-2013-2014)
LINK2. (http://www.moh.go.tz/index.php/newsroom/194-kada-za-afya-compiled-2014)



DIWANI WA C.C.M KOROGWE AJIUZULU!

Diwani wa Kata ya Mswaha Darajani, Tarafa ya Mombo wilayani Korogwe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Bwana Aweso Kipaku ameamua kuandika barua ya kujiuzuru kwa kile alichodai kuwa kudhalilishwa na Mkuu wa Wilaya Korogwe kwa kumuweka ndani.

Taarifa zilizozagaa ni kwamba sababu kubwa ya kukamatwa diwani huyo pamoja na mtendaji wa kijiji pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji ni madai kuwa wamekuwa wakichochea mgogoro kati ya wanakijiji cha Mswaha darajani na wafugaji wa kabila la Wamburu.
Diwani wa kata ya mswaha (CCM ) wilayani korogwe leo kafikishwa mahakamani pamoja na mwenyekiti na mtendaji wa kijiji cha Mswaha Darajani kwa tuhuma za kuchochea watu kuchoma moto mazizi ya wafugaji kata ya Mswaha.from facebook

No comments:

Post a Comment