Diwani wa Kata ya Mswaha Darajani, Tarafa ya Mombo wilayani Korogwe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Bwana Aweso Kipaku ameamua kuandika barua ya kujiuzuru kwa kile alichodai kuwa kudhalilishwa na Mkuu wa Wilaya Korogwe kwa kumuweka ndani.
Taarifa zilizozagaa ni kwamba sababu kubwa ya kukamatwa diwani huyo pamoja na mtendaji wa kijiji pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji ni madai kuwa wamekuwa wakichochea mgogoro kati ya wanakijiji cha Mswaha darajani na wafugaji wa kabila la Wamburu.
Saturday, January 25, 2014
Tuesday, January 21, 2014
Pata Historia ya Wilaya ya Korogwe Hapa
Historia ya Wilaya ya Korogwe
Wilaya ya Korogwe ilianza mwaka 1966 ambapo ilitenganishwa na Wilaya ya Lushoto. Kutokana na Wilaya ya Lushoto kuwa na eneo kubwa kiutawala, ilikuwa vigumu kutoa huduma kwa wananchi. Kabla eneo hili halijatengana na Wilaya ya Lushoto lilijulikana kama Korogwe “Sub-District” na mtawala wa eneo alikuwa ni “District Officer Incharge”.
Asili ya jina Korogwe ni jina la mmoja wa wakazi wa awali wa eneo hilo ambaye alijulikana kama Mkorogwe ambaye alikuwa ni Mzigua kwa kabila aliyeishi katika kitongoji cha Kilole- Kambi ya Maziwa. Mwaka 1966 Korogwe ilitangazwa kuwa Wilaya kupitia Tangazo la Serikali Na. 429 la Mwaka 1966 (GN No.429 of 1966). Mkuu wa Wilaya wa kwanza aliitwa Rajabu Semvua, wakati huo ilikuwa na Tarafa nne (4) ambazo ni Korogwe, Mombo, Bungu na Magoma kwa kuzingatia mfumo wa Kichifu uliokuwepo kabla ya Uhuru.
Kufuatia Tangazo hilo la Serikali ilianzishwa Halmashauri kamili iliyojulikana kama Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe. Mtendaji Mkuu wa Halmashauri kwa wakati huo alijulikana kama Mkurugenzi wa Maendeleo wa Wilaya (District Development Director- DDD) ambaye alishirikiana na Wakuu wa Idara mbalimbali katika kufanikisha utendaji kazi wa Ofisi yake. Katika jitahada za kusogeza huduma karibu na wananchi, Serikali kupitia Tangazo Na. 352 la tarehe 19/7/2004 ilianzisha Halmashauri ya Mji na kuifanya Wilaya ya
Korogwe kuwa na Halmashauri mbili (Halmashauri ya Mji na Wilaya). Wilaya ina eneo lenye kilomita za mraba 3,756 ambazo zimegawanyika katika Halmashauri ya Mji Korogwe yenye Kilomita za mraba 212 na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe yenye Kilomita 3,544. Halmashauri hizi zina Tarafa 5, Kata 28, Vijiji 139, Vitongoji 610 na Mitaa 17 na zinakadiriwa kuwa na jumla ya watu 324,020.
Wilaya ya Korogwe inapitiwa na barabara kuu inayoiunganisha na Miji mikubwa ya Dar-es- salaam, Arusha, Kilimanjaro, Pwani, Tanga Mjini, Morogoro na nchi za jirani ambazo ni Kenya na Uganda, hii inaifanya Korogwe kuwa Mji wa Kibiashara.
Subscribe to:
Posts (Atom)
